Rais
Paul Kagame wa Rwanda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa
Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayotarajiwa
kuanza Juni 28,2016 hadi Julai 8,2016 ambayo yatafunguliwa rasmi Julai
1,2016 na Rais huyo akiambatana na mwenyeji wake Rais Dk.John Magufuli.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Kaimu
Mkurugenzi wa TanTrade, Edwin Rutageruka alisema maonesho hayo yatatoa
fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi pamoja na taasisi
mbalimbali kutangaza biashara na huduma wanazotoa, kutoa fursa kwa
wafanyabiashara wa ndani kujifunza mambo ya biashara na uzalishaji bora
wa bidhaa kulingana na soko la kimataifa, kutengeneza jukwaa la
kibishara ambap hutoa fursa kwa wafanyabiashara kutengeneza mitandao ya
mawasiliano baina yao inayowasaidia kukuza biashara na kufikia malengo
waliyojiwekea na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kuuza bidhaa zao.
Rutageruka alisema nchi 30 zitashiriki maonesho hayo huku makampuni
yakiwa 650.
Alitaja
viingilio katika maonesho hayo kuwa kwa watoto itakuwa ni sh.1000 na
wakubwa sh.3000 hiyo ni kuanzia Juni 28n hadi Julai 8,2016 lakini katika
siku ya Julai 7, 2016 kwa wakubwa itakuwa ni sh. 4000. Kaimu Mkurugenzi
Mkuu huyo alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi na wafanyabiashara
kutumia fursa hiyo kutembelea kwenye maonesho hayo ili kujifunza mambo
ya biashara.