Wananchi wakitaharuki baada ya tukio hilo kutokea.
Nyumba moja iliyopo mtaa wa
Kiseke wilayani Ilemela mkoani Mwanza imeteketea kwa moto leo asubuhi na
kuunguza vitu vingi huku wakazi wa nyumba hiyo wakinusurika.
Taarifa zinaarifu kuwa, nyumba hiyo
imewaka moto baada ya mmoja wa watoto wa familia hiyo kuamka asubuhi na
kumwaga mafuta ya taa katika moja ya chumba cha nyumba hiyo na kisha
kuwasha moto.
Imeelezwa kuwa, kijana huyo ambaye
anadaiwa kuwa na matatizo ya akili amekuwa akiwatishia kwa muda mrefu
kuwachoma moto lakini wamekuwa wakimpuuza kutokana na matatizo yake ya
akili.