Jun 28, 2016

Lissu na wenzake wapandishwa kizimbani Dar

13511054_10209610213638192_5659084205571097646_nMbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (katikati) na Mhariri wa Mawio, Simon Mkina (wa poli kutoka kushoto mwenye miwani) na mchapishaji wao Ismail Mahboob (wa tatu kutoka kushoto mbele).
MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu  na Mhariri wa Mawio, Simon Mkina na mchapishaji wao Ismail Mahboob leo wamepandishwa tena mahakamani Kisutu, Dar  kwa uchochezi.
Kwenye shitaka hilo, Lissu pamoja na washitakiwa wenzake wanadaiwa kufanya makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchochezi kupitia Gazeti la Mawio la Januari 14,  2016.
Kwenye gazeti hilo lililoandikwa kichwa cha habari ‘Machafuko yaja Zanzibar’ Lissu alinukuliwa kama mchangiaji wa gazeti hilo ambapo tayari limefutwa na serikali.
Hii ni mara ya pili washitakiwa hao kupandishwa kizimbani. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 11, 2016.