Jun 21, 2016

KIKUNDI CHA UPENDO WOMEN'S GROUP CHA UBELGIJI CHATOA SHUKRANI KWA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UBELGIJI

Rais wa kikundi cha Upendo Women's Group ambaye pia ndiye mwenyekiti cha kikundi hicho Mh:Theresia Greca,ametoa shukrani za dhati kabisa kwa Rais mstaafu wa Tanzania Mh: Benjamin William Mkapa kwa kuwachangia kikundi chao,Shukrani za pekee kwa Kaimu Balozi wa Tanzania Mrs Agnes Kayola na Ubalozi mzima kwa mchango wao mkubwa wa kufanikisha zoezi zima la ufanikishaji wa fedha za kuisaidia hospital ya Mwananyamala nchini Tanzania.{picha na maelezo toka Maganga One Blog} 
Pichani wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali waliohudhuria sherehe za uchangishaji wa fedha kwa ajili ya hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam.Shukrani zinatolewa na wana Upendo Women's Group kwa ufanikishaji wa zoezi zima 
Baadhi ya Viongozi na wanachama wa Upendo Women's Group,kina mama wenye makazi yao nchini Ubegiji wametoa shukrani zao za dhati kabisaa kwa kila mmoja alishiriki vyema katika kufanikisha shughuli yao ya uchangishaji wa fedha kwa ajili ya kuisadia hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.Wana Upendo wanapeleka shukrani zao kwa Rais Mstaafu Mh:Benjamin William Mkapa kwa kujitolea mchango wake,Bila kusahau shukrani zao kwa Kaimu Balozi wa Tanzania Mrs Agnes Kayola na Ubalozi mzima wa Tanzania nchini Ubelgiji.Wanatoa shukrani kwa vikundi mbalimbali vya maonyesho na kila mmoja aliyefanikisha zoezi zima. 
Katika kuchangisha fedha ili kusaidia hospitali ya Mwananyamala nchini Tanzania, Upendo Women's Group waliaanda maonyesho mbalimbali ikiwemo na maonyesho ya mavazi.
Afisa Ubalozi Mr.Shayo {kushoto} pia nae alishiriki katika sherehe hizi fupi za uchangishaji wa pesa wa kuisaidia hospital ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam.Wana Upendo Group wanatoa shukrani zao za dhati kwa ushiriki na mchango wao mkubwa waliojitolea wa maafisa ubalozi wa Tanzania katika kufanikisha zoezi zima.