Jun 23, 2016

Dully Skyes hakufurahishwa na uwepo wa Joh Makini

Dully Skyes akiwa na TID studio.
Msanii TID ambaye siku za karibuni aliachia wimbo wake mpya 'Confidence' ambao amemshirikisha Joh Makini amefunguka na kusema kuwa kazi hiyo awali alikuwa amemshirikisha Dully SkyesMsanii TID ambaye siku za karibuni aliachia wimbo wake mpya 'Confidence' ambao amemshirikisha Joh Makini amefunguka na kusema kuwa kazi hiyo awali alikuwa amemshirikisha Dully Skyes lakini alifuta sauti ya Dully Skyes baada ya Dully kuona TID amemuongeza Joh Makini katika kazi hiyo.
Kwa mujibu wa TID alisema aliamua kufanya maamuzi ya kufuta sauti za Dully Skyes baada ya kuona amesusa kufanya video ya kazi hiyo kutokana na uwepo wa Joh Makini jambo ambalo lilimpelekea kufuta sauti zake ili abaki yeye na Joh Makini na maisha yaendelee.
Planet Bongo ilimvutia waya Dully Sykes kutaka kufahamu kama kweli alisusa kufanya video ya kazi hiyo baada ya kuona TID amemuongeza Joh Makini ndipo hapo Dully Skyes alipogoma kuzungumzia suala hilo na kusema yeye sasa amefunguka hayupo tayari kuzungumzia masuala hayo na kuongeza kuwa kama tunataka kuzungumza na yeye tuzungumze kuhusu kazi zake yeye ni si kazi za watu wengine.