Gari la polisi likiwasili eneo la tukio.
Dodoma;
JESHI la Polisi mkoani Dodoma
limewasambaratisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya mkoani humo ambao ni
wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa
wamekusanyika katika mahafali ya Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu
Chadema (CHASO) yaliyopangwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya
African Dream mjini humo ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mstaafu,
Mh. Fredrick Sumaye.
Polisi wakiwa wamezingira ukumbi huo.
Kwa mjibu wa maelezo ya Jeshi la Polisi
mkoani Dodoma, wanafunzi hao walifanya mkusanyiko usiokuwa halali kwa
kuwa hawakuwa na kibali cha kuwarushusu kukusanyika eneo hilo ndiyo
maana polisi wakaamua kuwasambaratisha ili kuzuia mikusanyiko ya kisiasa
isiyokuwa halali.
CHANZO: ITV