Dodoma
UKAWA kama kawa: Ndiyo lugha
nyepesi tunayoweza kusema, hii ni kutokana na Wabunge wa Kambi ya
Upinzani kuendelea kususia vikao vya bunge baada ya leo kutoka tena nje
ya ukumbi huo kimya kimya wakisusia kuhudhuria vikao vya bunge
vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson.
Wabunge hao leo wametoka bungeni bila
mbwembwe kama za jana ambapo waliziba midomo yao kwa karatasi na utepe
kisha kutoka nje ya ukumbi wa bunge hilo mjini Dodoma.
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa ambaye pia ni
Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema kuwa, kwa sasa
kamati ya uongozi ya umoja huo (UKAWA) imeingia kufanya kikao kujadili
mustakabali wao bungeni na kwamba watatoa taarifa kamili baada ya
kumalizika kwa kikao hicho.