Na Mwandishi wetu, RISASI MCHANGANYIKO
DAR ES SALAAM: Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania linaloendelea mjini Dodoma, likijadili bajeti ya
mwaka huu wa fedha, linaelezwa kuwa ni la ndivyo sivyo, Risasi linakuja
na taarifa kamili.
Wapinzani hao, chini ya umoja wao wa
Ukawa, wamekuwa wakidai kuwa Dk. Tulia anawaburuza kwa kutosikiliza hoja
zao na kwamba anatumia ubabe kupitisha au kuondoa baadhi ya hoja
zinazowasilishwa na wabunge wa kambi hiyo.
“Kama hawasikilizwi, hawana jinsi ya
kufanya, kutoka nje ya bunge ni namna inayokubalika kikanuni endapo
wabunge hawakubaliani na jambo, lakini kwa hiki kinachotokea, nadhani
uongozi wa bunge kwa ujumla wake, unapaswa kuwatazama zaidi wananchi
kuliko wabunge.
“Kama wapinzani wana matatizo na Dk.
Tulia, wangetumia busara, wenyeviti wangeongoza vikao vya bunge wakati
suluhisho likitafutwa, lakini kuendelea kumtumia naibu spika huyo ni
kama wanawafukuza makusudi wapinzani,” alisema Kohli Samson, mkazi wa
Mbagala.
Auness Jacob, mfanyabiashara wa vifaa
vya ujenzi wa Manzese jijini Dar es Salaam, licha ya kuwalaumu wapinzani
kwa kutoka nje kila mara, lakini alipongeza msimamo wa uongozi wa bunge
wa kuendelea kumtumia Naibu Spika Dk. Tulia kuongoza vikao vyake.
Alisema kuwatumia wenyeviti wa Bunge ni sawa na kunywea kwa wapinzani, kwani madai yao hayana msingi zaidi ya kutafuta umaarufu.
“Hawa hawana hoja, walianza na Bunge
Live, wameshindwa sasa wanaanza sarakasi zingine, sasa kama Dk. Tulia
atakaa pembeni, kesho wakisema hawamtaki Ndugai, naye akae pembeni? Huu
ni wakati wa kazi,” alisema na kuongeza kuwa hata hivyo, kutoka kwa
wapinzani kumepunguza msisimko wa majadiliano ya bajeti.
Kwenye mitandao ya kijamii, watu wengi
walionesha kupagawa na staili mpya iliyofanywa na wabunge wa upinzani,
ambao walifunga midomo yao kwa karatasi, zilizokuwa zimeandikwa ujumbe
mbalimbali.
Wabunge wa upinzani walianza kutoka nje
ya Bunge wakati wa uwasilishaji wa bajeti za wizara, wakipinga hatua ya
naibu spika kukataa hoja zao mbalimbali, ikiwa ni pamoja na miongozo na
taarifa, kwa walichosema anawaburuza