Jun 9, 2016

BENKI YA DTB TANZANIA YAZINDUA TAWI LA 25 JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi, akisaidiana na Mwenyekiti wa Banki ya Diamond Trust (DTB), Bw. Abdul Samji, kukata utepe katika uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo la CBD. Kushoto ni Bi. Nasim Devji Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo nchini, kulia ni Mwakilishi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Hezron Gyimri. Tawi la CBD linakuwa ni tawi la 25 la benki hiyo nchini Tanzania na la 11 jijini Dar es Salaam.

Benki ya Diamond Trust Tanzania, (DTB Tanzania),leo imezindua rasmi tawi la CBD lilipolo katikati ya jiji la Dar es Salaam kwenye jengo la Diamond Plaza, makutano ya barabara ya Samora na mtaa wa Mirambo. Tawi la CBD ni la ishirini na tano nchini na la kumi na moja katika jiji la Dar es Salaam.

Tawi la CBD litafunguliwa jumatatu hadi ijumaa, saa 2:30 asubuhi hadi saa 10:30 jioni na Jumamosi saa 3:30 asubuhi hadi sa 7:00 mchana.

Akihutubia katika hafla fupi iliyofanyika ndani ya benki, Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Raymond Mushi, alitoa pongezi kwa uongozi wa benki ya DTB Tanzania kwa ufunguzi wa takriban matawi mawili kila mwaka licha ya changamoto zinazokabili sekta ya fedha nchini na duniani kwa ujumla. Benki ya DTB imefanikiwa kufungua matawi ishirini na moja katika miji kumi na tatu ndani ya mika minane (2007 – 2016).