
Mkurugenzi
Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na mkakati wa uboreshaji wa mtandao unaofanywa na kampuni
yake. Anayetazama kulia ni Mkuu wa Zantel upande wa Zanzibar, Mohamed
Mussa.

Mkurugenzi
Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akisisitiza jambo wakati akizungumza
na waandishi wa habari kuhusiana na mkakati wa uboreshaji wa mtandao
unaofanywa na kampuni yake. Anayetazama kulia ni Mkuu wa Zantel upande
wa Zanzibar, Mohamed Mussa, na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel
upande wa Zanzibar, Ibrahim Attas.
Mkuu
wa Zantel upande wa Zanzibar, Mohamed Mussa akisisitiza jambo wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkakati wa uboreshaji wa
mtandao unaofanywa na kampuni yake. Anayetazama kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin.
Kampuni
ya simu inayoongoza visiwani Zanzibar, Zantel, imewekeza jumla ya dola
milioni 10 za kimarekani ili kuimarisha huduma zake za mawasiliano
nchini.Mpango huo unajumuisha kubadilisha mfumo mzima wa mawasiliano kwa
kubadilisha vifaa vilivyokuwepo na kuweka mitambo mipya kwa madhumuni
ya kuimarisha mawasiliano ya simu na kuongeza kasi ya mtandao.
Akizungumza
na waandishi wa habari visiwani humu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel,
Bwana Benoit Janin alisema kuimarisha huko katika huduma za simu na
mtandao kwa upande wa Zanzibar ndio kilikuwa kipaumbele cha kwanza cha
kampuni ya Zantel.‘Kampuni ya Zantel imeanza safari mpya kabisa yenye
lengo la kuimarisha na kurudisha nafasi ya mtandao wa Zantel katika
ubunifu na kutoa huduma bora visiwani hapa’ alisema bwana Janin.Bwana
Janin pia alisema uboreshaji wa huduma za Zantel ni mpango endelevu na
katika kipindi kifupi kijacho, Zantel itaendelea kufunga vifaa vipya
hali ambayo itawafanya wateja waweze kuwasiliana kwa bei nafuu na bila
ya bughudha.
‘Maboresho
haya yamelenga kuhakikisha tunakuza na kuimarisha teknolojia ya
mawasiliano ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za kipekee na kutekeleza
ahadi yetu ya kuendelea kuongoza katika kutoa huduma bora kwa wateja
wetu’ alisema Bwana Benoit.Janin pia alielezea mpango wa kampuni ya
Zantel kuboresha huduma ya EzyPesa kwa kurekebisha mfumo mzima ili uweze
kuhimili mawakala wengi na kuongeza huduma za ndani ya mfumo huo.
Katika kipindi kifupi pia kampuni ya Zantel pia imefanikiwa kuondoa
mtandao wa 2G na kuweka mtandao wa 3G, sambamba na kuzindua rasmi
mtandao wa kasi wa intaneti wa 4G mjini Unguja.
‘Nina
furaha kubwa jinsi utekelezaji wa mikakati yetu unavyoendelea wa
kuboresha huduma zetu ambao utawapa wateja wetu nafasi ya kufurahia
huduma zetu na pia kuwapunguzia gharama za mawasliano huku tukukidhi
mahitaji ya wateja wetu kwa wakati huu na siku zijazo’ alisema Janin.
Bwana Janin pia alisema tayari matatizo ya mawasiliano ya huduma za 3G
yameshatatuliwa kwa kutumia mkonga wa fiber katika ya maeneo ya Unguja
na Pemba.
‘Tumefanikiwa
kuyatatua matatizo madogo madogo katika mji mkongwe kwa kuweka vifaa
ambavyo vimesaidia sana kuondoa msongamano wa mawasiliano majumbani na
katika sehemu za wazi’ alisema Janin. Kampuni ya Zantel ambayo ilizindua
huduma ya mtandao wa 4G katika mji wa Unguja mwezi uliopita pia
imefanikiwa kufikisha mawasiliano kwa asilimia 80% ya watanzania kutoka
asilimia 40% waliyokua wanawafikia awali.
