
Wanafunzi wa chuo kikuu cha cha Dar es
salaam mpaka sasa wamegoma wakiishinikiza bodi ya mikopo kutoa fedha
kwa ajili ya kujikimu.
Makamu wa Rais wa serikali ya
wanafunzi, Shamila Mshengema amesema mgomo huo ni matokeo ya taarifa
zisizoeleweka zilizo kuwa zikitolewa na bodi juu ya lini fedha hizo
zitatolewa.
Kwa kawaida pesa ya chakula huingiziwa kila baada ya siku 60 na mpaka sasa yapata wiki mbili pesa hiyo haijaingizwa.
Mgomo huo unakuja zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Rais Magufuli Kuzulu chuo hicho kwa ajili ya uzinduzi wa jengo la Maktaba