Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles John Mwijage
akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Mfuko wa
Pensheni wa PFF mara baada ya kufungua maonyesho ya biashara ya
kimataifa ya Tanga yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwakidila jijini
Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa Tanga, Jabir Bundile akiwa kwenye banda lao lililopo kwenye maonyesho hayo.
Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa Tanga, Jabir Bundile wa
pili kulia akitoa elimu kwa mkazi wa Tanga namyanatolewa na mfuko huo.
WAKAZI
wa Mkoa wa Tanga wametakiwa kutumia fursa ya kujiunga na Mfumo wa wote
scheme unaotolewa na Mfuko wa Pensheni PPF ili kuwawezesha kukithi
mahitaji kwa sababu unalengo kuu la kutambua mchango wa ushiriki kwenye
sekta isiyo rasmi katika kuinua uchumi.
Hayo yalisemwa jana na Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa
Tanga, Jabir Bundile wakati alipozungumza na gazeti hili katika
maonyesho ya nne ya biashara ya kimataifa ya Tanga yanayofanyika kwenye
viwanja vya Mwakidila jijini hapa ambapo alisema mfumo huo utasaidia
kufikia wananchi wengi.
Alisema kuwa fao hilo likuwa likitoa fursa mbalimbali kwa
wafanyakazi waliopo kwenye sekta iliyo rasmi na isiyorasmi ili
kuwawezesha kunufaika na mfumo huo kwa ajili ya kukuza shughuli
mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa mustakabali wa maendeleo yao.
“Niwaambieni kila mtu au kikundi chenye mlengo wa kiuchumi
kilichopo kwenye sekta isiyorasmi kama vile wakulima, wafugaji, wavuvi,
mama lishe, waendesha pikipiki, wajasiriamali wadogo wadogo kwa lengo la
kuhakikisha wananufaika kupitia mfumo huo “Alisema.
Aliongeza kuwa pia mfumo huo unawagusa wasanii, wana michezo,
wachimbaji madini wadogo wadogo wanaweza kujiunga na mfumo huo kwa lengo
la kupata manufaa yanayotokana na mfuko huo.
Sambamba na hilo pia alisisitiza uwepo wa mafao yanayotolewa na
mfuko huo kuwa ni ule wa Afya, Fao la Uzeeni, Mkopo wa elimu ambao
unalengo la wanachama kukopa na kujiendeleza kielimu na PPF na mkopo
ambao unakuwezesha kutimiza ndoto yako.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha