May 30, 2016

Airtel yatoa msaada wa Kompyuta 30 kwa chuo cha taifa cha utalii

Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (Kulia) akizungumza na vyombo vya habari wakati wa hafla ya makabidhiano ya kompyuta 30 kwa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa, akishuhudiwa na Meneja Msaidizi wa chuo Oscar Mwambene (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Mafunzo Eunice Nderingo Ulomi (kushoto), hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo Temeke, Dar es Salaam.

  Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) akikabidhi kompyuta 30 kwa Meneja Msaidizi wa chuo cha Taifa cha Utalii (NCT)  Oscar Mwambene (katikati)   kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa, akishuhudiwa na Mkurugenzi wa Mafunzo Eunice Nderingo Ulomi (kushoto) katika hafla iliyofanyika chuoni hapo Temeke, Dar es Salaam.
 Mkuu wa idara ya Utalii katika Chuo cha Taifa cha Utalii Elina Makanja (Kushoto) akimwelekeza mwanafunzi Agape Gerald (Kulia) mara baada ya kukabidhiwa kompyuta 30 kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa, akishuhudiwa na Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (Katikati).