
Waziri wa
ujenzi, uchukuzi na mawasiluano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na
wafanyakazi wa kampuni ya simu ya TTCL wa Mkoa wa Kigoma alipowasili
ofisini kwao.

Mtendaji mkuu
wa kampuni ya TTCL nchini Dk Kamugisha Rwezaura (wa kushoto) akiongea
na mbunge wa Kigoma mjini Zitto kabwe nje ya viwanja vya ofisi za
kampuni hiyo Kigoma, katikati ni waziri wa ujenzi, uchukuzi na
mawasiliano profesa Makame Mbarawa.

Waziri wa
ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbawala akiongea na
watendaji wa kampuni ya simu ya TTCL Kigoma alipokuwa akiangalia mtambo
wa mkongo wa Taifa kwenye ofisi za kampuni hiyo Kigoma.
Na Editha Karlo, wa blog ya jamii, Kigoma
KAMPUNI
ya Mawasiliano ya simu Tanzania TTCL imeiomba serikali kuwamilikisha
mkongo wa mawasiliano wa Taifa ilikampuni hiyo waweze kuuendesha wao
kutokana na uwezo walionao na mafundi na wataalamu wa kutosha.
Ombi hilo
lilitolewa na meneja wa TTCL Mkoani Kigoma,Abdalah Lugage wakati akitoa
taarifa ya Mkoa kwa Waziri wa ujenzi uchukuzi na Mawasiliano wakati
alipotembelea ofisi hizo. Alisema
shirika hilo linauwezo wa kusambaza mawasiliano katika ofisi zote na
mpakasasa wamefikia uwezo wa internet 4G ambayo inatumiwa na ofisi zote
za serikali na binafsi.
Lugage
alisema wao kama Shirika la mawasiliano wanauwezo wa kumiliki mtambo
huo wa taifa kutokana na uwezo mkubwa na kazi nzuri wanayo ifanya
kuwahudumia watanzania katika mawasiliano.
Waziri wa
ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano,Makame Mbarawa alisema Serikali haiwezi
kuwaachia TTCL kumiliki mkonga Wa taifa kwa asilimia zote jambo
linaloweza kupelekea Makampuni mengine kuja kununua Mkongo na kuuwa
shirika.
Mbarawa
alisema atajalibu kuongea na Serikali na Viongozi ikiwezekana serikali
imiliki 30% na shirika hilo kumiliki 70% ya Mkongo wa Taifa ilikuyafanya
makampuni mengine kutumia Mkongo wa Taifa na serikali kujiingizia
mapato kupitia Mawasiliano.
"Kuhusiana
na suala la Mkongo wa Taifa nitaongea na TCRA muweze kuingia kwenye
ubia na serikali katika umiliki wa Mkongo wa Taifa naniwatake mboleshe
kwanza mikongo na mitambo yenu ilitujilizishe na Uhuma zenu "'alisema
Mbarawa.
Mbarawa
alisema pia Serikali inampango wa kuboresha ubora wa internet kufikia
masafa ya 800 ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuifanya shirika hilo kufanya
kazi kwa uhakika zaidi. Aidha
amewaomba watumishi wote waweze kufanya kazi kwa umakini na ushirikiano
ilikuweza kutoa huduma zenyeufanisi na umakini wa hali ya juuu.
Kwa
upande wake Afisa mtendaji mkuu wa TTCL nchini Dr Kamugisha Kazaura
alisema serikali inampango wa kuiboresha kampuni hiyo ilikuweza
kuwarahisishia Watanzania huduma za Mawasiliano. hivyo
aliwaahidi watanzania shirika hilo limejipanga ipasavyo kuhakikisha
huduma hizo zinaboreshwa na Wanatanzania wanapata huduma zenyeviwango
vya kujitosheleza.