Apr 30, 2016

Trump ni Miongoni Mwa Watu 100 Wanye Ushawishi Mkubwa Duniani

kim_jong-un_watch_test_640x360_reuters_nocredit
Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong un
RAPA maarufu wa Marekani Nicki Minaj, rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong un, msaka tiketi ya kuwania urais Marekani kwa tiketi ya Republican Donald Trump na Lewis Hamilton wana kitu kimoja kinachowaunganisha. Huwezi kufikiria kwamba wanaweza kuketi katika meza moja, lakini wametajwa miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani.
donald-trump-wants-to-wage-economic-war-on-mexico-to-get-them-to-pay-for-a-border-wall 
Donald Trump
Orodha hiyo ya mwaka 2016 pia inamshirikisha Hillary Clinton, Kendrick Lamar, PewDiePie, Adele, Caitlyn Jenner na Leonardo DiCaprio.
Katika tamasha la siku ya Jumanne la New York baadhi ya nyota hao walihudhuria. Nicki alisema kuwa hiyo inatokana na yeye kuwa mwanamke huru huku akiwaambia wanaume waliojaa katika ukumbi wa tamasha hiyo kwamba: iwapo hamjui kuwashughulikia wanawake wenu kuna watu 100 ambao wana uwezo wa kuchukua fursa hiyo.
Nicki_Minaj
Nicki Minaj
Lewis Hamilton alisema kuwa ni heshima kubwa kwake kuorodheshwa katika tamasha hiyo ya watu 100 mbali na kuorodheshwa miongoni mwa watu 100 duniani walio na ushawishi mkubwa.
Wakati huohuo alimuomboleza marehemu Prince akisema kuwa alikuwa mwanamuziki bora wa kizazi chote