
Jumla
ya watoto 120 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya
Bugando jijini Mwanza, kufuatia tatizo la kichwa kikubwa walilozaliwa
nalo chini ya udhamini wa taasisi ya GSM ambayo imedhamini zoezi hilo
litakalofanyika katika mikoa mitano ikiwa ni awamu ya kwanza kati ya nne
zinazotarajiwa kufanyika tanzania nzima.

Mtaalamu
wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya Fahamu, Dk Gerald Mayaya akitoa
ufafanuzi kwa wanahabari kuhusiana na kambi ya upasuaji wa watoto wenye
vichwa vikubwa katika Hospitali ya Bugando

Meneja
Mkuu wa taasisi ya GSM, Shannon Kiwamba (katikati) akiongea na
wanahabari kuhusiana na sera yao mpya ya kusaidia watanzania katika
masuala ya elimu na Afya, kulia kwake ni Mkuu wa Hospitali ya Bingando,
Prof Kien Mtena na kushoto kwake ni Mkuu wa mawasiliano wa Taasisi ya
GSM, Halfan Kiwamba

maelezo ya ufafanuzi yakiendelea kutolewa na Halfan Kiwamba(Wa pili kutoka kushoto) kutoka GSM Foundation.
Akiongea
na waandishi wa habari katika uzinduzi wa zoezi hilo linalojumuisha
madaktari Bingwa 10 kutoka Taasisi ya mifupa na Upasuaji MOI, Mkurugenzi
Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Profesa Kien Mteta aliishukuru taasisi ya
GSM kwa kuamua kulichukua tatizo hilo ambalo ameliita kuwa ni kubwa
ukilinganisha na jinsi linavyochukuliwa na jamii ya watanzania.
Dk
Kien aliwaambia wanahabari kwamba jumla ya watoto 2000 huzaliwa na
vichwa vikubwa katika kanda ya Ziwa peke yake, na mtaalamu wa kuhudumia
wagonjwa wa namna hii ni mmoja tu ambapo pia kwa Tanzania nzima,
wataalamu wa upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa wako tisa tu.
Cha
kusikitisha ni kwamba kati ya hao, ni wachache sana hurudi kwa ajili ya
matibabu bali wengi wao hufariki kwa kufichwa ndani na wazazi wao aidha
kwa imani za kishirikina ama kushindwa kwa wazazi kumudu gharama za
matibabu.
PICHANI
JUU: Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Profesa Kien Mteta(kushoto) akiongea
na wanahabari huku akisikilizwa kwa umakini na Halfan Kiwamba(kulia) na
Mkurugenzi wa taasisi ya Mifupa na upasuaji Dk Othman
Kiloloma(katikati)