MBUNGE wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema)
pamoja na Diwani wa Kimanga Manase John Mjema wamepandishwa kizimbani
leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar
na kusomewa shtaka la kumjeruhi Theresia Mbaga kwenye ukumbi wa Karimjee
mnamo Februari 27 mwaka huu.
Mmbando alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji la
Dar es Salaam uliofanyika kwenye Ukumbu wa Kareem Jee na baadaye
kuahirishwa hatua ambayo iliibua malumbano.
Mbele ya Cyprian Mheka, Hakimi Mkazi Kisutu washitakiwa hao
walikana kosa hilo ambapo hakimu alighairisha kesi hiyo mpaka tarehe 16
Machi mwaka huu.
Kubenea na Mjema wote wamekana shtaka na kujidhamini wenyewe baada ya kusaini dhamana ya shilingi milioni mbili kila mmoja.
Washtakiwa wengine katika shtaka hilo
ni Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima James Mdee, Mbunge wa Jimbo la Ukonga
Mwita Mwikabe Waitara na wengine wawili.
Jana asubuhi kwenye mahakama hiyo
Kubenea akihudhuria kesi yake dhidi ya Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, alikamatwa na Jeshi la Polisi na kuwekwa chini ya ulinzi