Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo wa NMB - Abdulmajid Nsekela akiongea
na wafanyabiashara kwenye hafla ya wajasiliamali ambao ni wateja wa NMB
wa wilaya ya Kinondoni.

Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni Mh. Paul Makonda akiwa kwenye picha ya
pamoja na washiriki wa hafla ya Business Club iliyofanyika Sinza jijini
Dar es Salaam

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam - Vicky Bishubo akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni
NMB imekuwa ikuwakutanisha wafanyabiashara
wakubwa na wadogo walio
kwenye mtandao wa NMB Business Club kwaajili ya kuongea nao na kupokea
maoni yao na mrejesho wa jinsi gani benki inaweza kuboresha huduma kwa
wateja zaidi ya wajasiliamali 300 walihudhuria katika hafla iliyofanyika
jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi alikuwa
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni – Mh Paul Makonda.
NMB
Yatoa Mafunzo Ya Kijasiriamali Kwa Wafanyabiashara Wakubwa Na Wadogo
Nchini .Benki ya NMB PLC imetoa mafunzo ya kijasiriamali kwa zaidi ya
wafanyabiashara 300 jijini Dar es Salaaam. NMB ina jumla ya vilabu vya
biashara 34 nchi nzima vyenye wanachama zaidi ya 10,000. NMB
Business Clubs zina malengo ya kuwafikia jamii ya wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa ambao wanajumuisha wafanyabiashara zaidi ya 50,000 ambao ni wateja wa NMB nchi nzima.
Benki ya NMB PLC imekuwa kipaumbele kuhamasisha wanafanyabiashara nchini kujikimu kimaisha kwa kufungua vituo vya biashara nchini kimoja ambacho kipo kwenye wilaya ya Kinondoni- Sinza Business
Centre. Vituo hivi sio sehemu tuu ya kuchukulia mikopo bali pia ni sehemu ya wafanyabiashara kupata ushauri kuhusu mikopo na biashara kutoka kwa wa wataalamu wetu. Kaimu Afisa wa Wateja Wadogo wa Benki ya NMB PLC alisisitiza kwamba lengo kuu la vilabu hivi vya
biashara vimeundwa kuhakikisha wafanyabiashara nchini wanakuza mitaji yao, kuajiri watanzania wengi zaidi na pia kuchangia uchumi wa taifa hili kupitia ulipaji kodi.
Akiongea na wafanyabiashara nchini Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni Paul Makonda ameipongeza benki ya NMB kwa kuonyesha shauku ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi kupitia vilabu vya biashara ambavyo vinawapa wananachi elimu ya kijasiriamali na hivyo kupiga hatua ya kuiuchumi kimaisha.