Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla amekutana na baadhi ya Madaktari waliohitimu mafunzo
kwa vitendo kipindi cha 2014/2015 waliofika katika Wizara hiyo kwa lengo
la kujua hatima na mustakabali wa mambo mbalimbali ikiwemo suala la
ajira.
Madaktari
hao walioweza kuonana na Dk. Kigwangalla ni baadhi tu ya wawakilishi
wa Madaktari wengine ambapo kupitia viongozi wao wamebainisha kuwa,
kuwa kama wazarendo wapo tayari kuisaidia Serikali katika suala la tiba
nchini hasa kwendana na hali ya kauli mbiu ya hapa kazi hivyo kupitia
mazungumzo yao hayo na Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla na jopo la viongozi
wa Wizara hiyo, madai yao na masuala mengine wana Imani kubwa madai yao
yatashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi.