
Mashimo wa Barabara eneo la soko la Mapinduzi kama panavyoonekana katikaka picha, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda leo jijini Dar es Salaam alipotembelea na kuagiza patengenezwe haraka iwezekanavyo.

Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiangalia ubovu wa barabara ya
Mwanachamala 'A' hadi Makumbusho jijini Dar es Salaam leo.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amefanya ziara ya kukagua barabara
ya Mwanayama 'A' hadi Makumbusho ambayo imeharibika kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha.
Akizungumza
baada ya kukagua barabara hizo amewapa watendaji wa manispaa ya
Kinondoni wiki mbili kushughulikia tatizo hilo kutokana na adha ya
magari yanayotumia barabara hiyo.
Amesema kuwa kuharibika kwa barabara nyingi katika manispaa hiyo ni kutokana na kujenga chini ya kiwango.
Makonda
amesema fedha zinatolewa kwa ajili ya ujenzi lakini baadhi ya watendaji
wanajenga chini ya kiwango na kuwapa adhabu wananchi wanatumia barabara
hiyo ikiwemo na gari za kubeba.
Aidha amesema kuwa watahakikisha barabara zinafanyiwa maboresho katika urahishaji wa usafiri katika Manispaa ya Kinondoni.