Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na
Maafisa Wandamizi wa Jeshi la Polisi nchini kabla ya kufungua Mkutano wa
Mwaka wa Jeshi hilo, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliwataka Maafisa
hao kutoka Mikoa yote nchini kufanya kazi kwa kasi inayoandana na
Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na
uhalifu nchini. Watatu kulia meza kuu ni Inspekta Jenerali wa Polisi
(IGP), Ernest Mangu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akitoa hotuba yake kwa
Maafisa Waandamizi wa Jeshi lake, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) kuzungumza na maafisa hao
kutoka mikoa yote nchini na kuufungua Mkutano wao wa Mwaka unaofanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es
Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga kabla ya kufungua mkutano
huo, aliwataka Maafisa hao kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali
ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu
nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akimshukuru
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB nchini, Ineke Bussemaker, mara baada ya
kumkabidhi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kulia),
Shilingi Milioni 75 kwa ajili ya kuudhamini Mkutano wa Mwaka wa Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Polisi kutoka Mikoa yote nchini. Mkutano huo
ulifunguliwa na Waziri Kitwanga katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, na aliwataka Maafisa hao
kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia
wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini.