Naibu Waziri maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Dkt.hamisi kigwangwala akizungmza na watumishi wa Afya.
Baadhi
ya wafanyakazi wa bohari ya dawa(msd)kanda ya kaskazini wakimsikiliza
naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto(hayupo
pichani)
watumishi mbalimbali wakifuatilia hotuba ya naibu waziri.(Habari na picha toka wizara ya afya)
………………………
Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuacha kuhujumu dawa zinazopelekwa kwa ajili ya wananchi na si za biashara kama wanavyofanya
Onyo
hilo yamesemwa mwishoni mwa wiki na naibu waziri wa afya,maendeleo ya
jamii,jinsia,wazee na watoto,dkt.hamisi kigwangwalla wakati akiongea na
wafanyakazi wa bohari ya dawa(msd)pamoja na wale wa hospitali ya mkoa ya
mount meru.
Dkt.
Kigwangwalla alisema serikali ya awamu ya tano yenye kaulimbiu ya “hapa
kazi tu”haitawavumilia watumishi wa aina hiyo na kama wapo basi waanze
kujipima kabla rungu la dola halijawafikia
Aidha,alisema
suala la upatikanaji wa.dawa kwa wananchi na kwa bei nafuu ni moja ya
mambo yaliyopewa kipaumbele katika serikali ya awamu ya tano
“Wananchi
wanatakiwa kupata dawa sahihi,kwa bei nafuu na kwa wakati,ndo maana
serikali imeamua kufungua maduka ya dawa ya ndani ya hospitali,Hii ni
moja ya malengo yaliyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya chama cha
Malibu”
Hatahivyo
aliongeza kuwa katika kudhibiti upotevu wa draws nchini,serikali
imeanza kutekeleza uwekaji nembo ya GoT katika vidonge vyote”na mimi
nawapa changamoto ya kuweka mkakati wa kuweka rangi Maalum ‘colour code’Kwa dawa zote zinazokuwa zimenunuliwa na serikali,sambamba na huo mkakati wenu wa nemo Licha
ya hivyo aliwataka wakuu wa hospitali,vituo vya afya pamoja na zahanati
wasipokee dawa bila kuwepo kwa kamati ya afya ambayo ndio wawakilishi
wa wananchi wa mahali husika ili kusiwepo na udanganyifu na kwenda
kwenye mfumo usio rasmi pamoja na kuzibandika dawa.zilizopokelewa kwenye
mbao.za matangazo Aliitaka bohari ya dawa(msd)kukamilisha
uwekaji nembo dawa zilizosalia na wawe na utaratibu wa kusimamia na
kukagua kama dawa Za.serikali zimefika.hadi sasa vidonge vipatavyo 65
vimekwishawekewa nembo ya GoT.