wanachama wa chama cha waajiri pamoja na wasio wanachama wa
wakiwa wanajadili kwa makini changamoto ambazo zinawakabili waajiri na
jinsi ya kuzitatua .
Na Woinde Shizza,Arusha
Chama
cha Waajiri nchini kimelalamikia vitendo vya rushwa kuwa vikwazo katika
biashara hivyo wameiomba serikali kukemea vitendo vya rushwa pamoja na
urasimu ili kuboresha mazingira mazuri ya biashara za kitaifa na
kimataifa.
Hayo
yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waajiri (ATE),Aggrey
Mlimuka akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Waajiri amesema kuwa
serikali inapaswa kujenga mazingira bora kwa waajiri wanaotoa nafasi
za ajira ili kujenga uchumi endelevu wa nchi
Mkurugenzi
huyo ameiomba serikali iondoe vikwazo kwa waajiri wanaoajiri wataalamu
kutoka nje kutokana na kukosekana kwa wataalamu hao nchini pamoja na
kupunguza tozo kubwa za mafunzo ya wafanyakazi ambayo ni asilimia 5%.
Kwa
upande wake Afisa Mwajiri wa Kampuni ya Utalii amesema kuwa kwa muda
mrefu wamekua wakipata adha kubwa wakati wa kuajiri watu kutoka nje ya
nchi suala ambalo serikali inatambua kuwa baadhi ya taaluma hazipatikani
nchini hivyo kulazimika kuchukua wataalamu kutoka nje.