“...Tunapenda
kuwathibithia Wateja wetu wote wa ndani na nje ya nchi, wadau wetu na
Umma kwa ujumla kwamba, taarifa hizi si sahihi, na kwamba mifumo yetu ya
Mawasiliano ya TTCL ipo salama, huduma zetu zote zipo thabiti na mpaka
sasa tunapotoa taarifa hii, hakuna uhalifu wowote uliofanyika kwa sisi
wenyewe kama Kampuni wala kwa mteja wetu yeyote,” alisema Thomas Mushi.
Aidha,
tunapenda kuwathibitishia kuwa, taarifa za Wateja wetu wote ikiwemo
Serikali , Idara, Wakala na Taasisi za Umma, Taasisi za fedha,
Mashirika, Makampuni na Watu binafsi zipo salama kabisa. Ukweli huu
unathibitishwa na Wateja wao pia kwani hadi sasa, hakuna hata mmoja
aliyeleta taarifa za kukosa huduma ama kupata athari zozote kutokana na
tetesi hizo.
Hata
hivyo, alisema pamoja na taarifa hizo, Wataalamu wa kampuni hiyo
wanaendelea kuwa macho kwa muda wote, ili kuhakikisha kuwa, wanafanyia
kazi kila taarifa ama tishio la kiusalama linaloweza kujitokeza katika
mfumo wao. “TTCL inaendelea kuwaomba Umma na Wateja wetu wote kuendelea
na majukumu yao kama kawaida bila wasiwasi wowote. TCCL inawaleta
Karibu.”
Alisema
Thomas Mushi. Kwa upande wake Meneja wa Kitengo cha Usalama Mifumo ya
Mawasiliano ya TTCL, Lina Rujweka alisema kitengo chao baada ya tetesi
hizo kimefanya uchunguzi wa kina na hakuna ashirio lolote la mifumo yao
kuingiliwa (kudukuliwa) kama ilivyoelezwa. Alisema kitengo hicho kina
wataalam ambao muda wote wapo kazini kufuatilia ufanisi wa mfumo wa
mawasiliano wa kampuni yao hivyo kuwaondoa hofu wateja wao.
“...
Baada ya taarifa hizo Kitengo cha Usalama wa Mifumo ya Mawasiliano ya
Kampuni ya TTCL kiliingia kazini ili kubaini ukweli wa taarifa hizo na
kufanya majaribio ya kitaalamu ili kuthibitisha usalama wa mifumo yetu.
Baada ya utafiti wa kina na majaribio ya kitaalamu, tunapenda
kuwathibithia Wateja wetu wote wa ndani na nje ya nchi, wadau wetu na
Umma kwa ujumla kwamba, taarifa hizi si sahihi...” alisema.