Na Anitha Jonas – MAELEZO.
Shirika
lisilo la kiserikali la Tanzania Feminist and Youth Change Organization
(TAFEYOCO) limemuomba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kuanzisha utaratibu wa kukutana na vijana ili kujadiliana mambo
mbalimbali.
Hayo
yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Shirika hilo Bw. Elvis Makumbo alipokuwa
akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam katika
mkutano uliyolenga kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
kwa kazi nzuri aliyoifanya katika siku mia moja za uongozi wake.
“Vijana
kwa sasa katika taifa ni wengi na ndiyo wenye uwezo wa kuleta maendeleo
katika nchi na nguvu kazi ya Taifa na wanachangamoto nyingi hivyo
Mheshimiwa Rais akijaribu kukutana nao nakuwasikiliza matatizo yao
itasaidia kuleta mafanikio katika nchi na kujua nini kifanyike kuleta
maendeleo katika Taifa,” alisema Bw. Makumbo.
Ameleza
kuwa, Mheshimiwa Rais ameonyesha moyo wadhati wa kuwatumikia wananchi
kwa kuwawajibisha watu wote walionekana wakitumia vibaya madaraka yao na
kufanya ubadhirifu wa pesa za umma kinyume na taratibu za kiutumishi wa
umma.
Mbali
na hayo Bw.Makumbo amemuomba mheshimiwa Rais kufikiria kuanzisha mfumo
au taasisi itakayohakiki mali za mtumishi wa umma na kuhoji ni namna
gani mali hizo amezipata ili kupunguza wimbi la watumishi wa umma wanao
tumia fedha za serikali vibaya kwa kujinufaisha wenyewe huku wakijiwekea
utajiri mkubwa usiyolingana na kipato chao.
Mwenyekiti
huyo aliendelea kumwomba Mheshimiwa Rais kuzidi kuzingozea nguvu
taasisi za Serikali ili kuzijengea uwezo mkubwa wa kiutendaji mfano wa
Taasisi hizo ni TAKUKURU na nyinginezo zinazosimamia mambo mbalimbali
Yenye tija kwa Taifa.
Shirika
hilo limesema Kauli Mbiu ya Mheshimiwa Rais ya Hapa Kazi Tu imeongeza
hari kubwa ya utendaji kwa wananchi kwa kuwahimiza kuwajibika ikiwemo
kwa watu wa sekta binafsi na taasisi za umma.