Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: MUIGIZAJI mkongwe wa
filamu Bongo, Blandina Chagula anayefahamika kisanii kama Johari,
anadaiwa kuwewesekea penzi la mbunge mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania (jina linahifadhiwa) ambaye alifunga ndoa miezi michache
iliyopita.
Chanzo makini kilicho karibu na msanii
huyo kimeliambia gazeti hili kuwa Johari alikasirishwa na kushangazwa na
hatua ya msanii mwenzake kuolewa na mbunge huyo, ilihali akijua kuwa
yeye aliwahi kuishi naye kimapenzi, ingawa alikataa kuolewa naye kwa
kile alichosema ‘hajatulia’.
“Johari anaweweseka kweli jamani, yaani
kinachomuuma huyo mke wa mheshimiwa ni yeye ndiye aliyemkutanisha na
anajua kila kitu, lakini anashangaa hata ilivyokuwa hadi akakubali
kuolewa naye, yaani ni kama mtu aliyeumia sana,” kilisema chanzo hicho
ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake ili kulinda ushoga wao.
Baada ya kunasa ushahidi unaothibitisha
Johari akimzungumzia mbunge huyo kuonesha anaweweseka, gazeti hili
lilimtafuta Johari na kumwuliza kuhusu tuhuma hizo, lakini msanii huyo
aliruka kimanga, akidai hajawahi kuweweseka kwa penzi la mbunge huyo na
wala hajawahi kuwazungumzia