Katibu
Mkuu Chama cha NRA Tanzania Bara Hassan Almasi Kisabya (wa pili
kushoto) akitoa tamko la chama chake kushiriki uchaguzi wa marudio
Zanzibar March 20 ya waandishi wa Habari(Hawapo Pichani)leo Jijini Dare s
salaam katika ukumbi wa Habari Maelezo.
Baaadhi
ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano ulioitishwa na Chama cha NRA
kuelezea ushiriki wao katika uchaguzi wa marudio Zanzibar.
Na Nyakongo Manyama MAELEZO
Chama
Cha National Reconstruction Alliance (NRA) kutoka
Zanzibar kimethibitisha kushiriki uchaguzi wa marudio wa Zanzibar
unaotarajiwa kufanyika Machi 20, mwaka huu baada ya kikao kilichofanyika
Februari 15.
Hayo
yamebainishwa na Katibu Mkuu Tanzania Bara Hassan Almasi Kisabya
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam
ambapo amesema kuwa Chama hicho kitashiriki uchaguzi wa marudio na
kusisitiza kuwa tamko lililotolewa na mgombea wao la kutoshiriki
uchaguzi wa marudio lipuuzwe kwani ni tamko lake binafsi na sio msimamo
wa chama.
“Tamko
lililotolewa tarehe 14/02/2016 Si Tamko la chama cha NRA bali ni tamko
binafsi na wale waliomuagiza kwani yeye hana mamlaka ya kukisemea chama
wala wagombea wengine wa chama pasipo Baraka na vikao halali vya chama”
alisema Kisabya.
Amesisitiza kuwa
maamuzi ya chama ni sharti yatoke katika chama na sio kwa mgombea na
ikiwa yeye amejitoa anatakiwa afuate taratibu za kisheria katika kujitoa
kama alivyofuata sheria katika kugombea nafasi hiyo.
Aidha,
Chama kinatoa taarifa kwa wagombea wote Zanzibar kujiandaa na wapiga
kura kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi
20, mwaka huu ili kutimiza haki yao kikatiba na kuchagua viongozi wao
kwa kipindi cha miaka mitano ijayo
Chama
cha NRA ni miongoni mwa vyama 14 vilivyosimamisha wagombea katika
uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar
uliofutwa kwa nafasi ya Rais.