
Mbunifu
wa Mavazi Amina Plummer Akitoa Mada kwenye Semiana ya Ujasiriamali kwa
Wanawake wa Zanzibar yenye Lengo la Kuwafundisha Mbinu Mbalimbali za
Biashara pamoja na Matumizi Sahihi ya Vipodozi Pendwa vya Luvtouch.
Mbunifu
wa mavazi Amina Plummer amewaasa wanawake wa zanzibar kujikita kwenye
ujasiriamali kwa kuwa ndio njia pekee ya kumkomboa mwanamke.amesema
ajira nyingi zimekuwa na ubaguzi na pili ni nafasi chache sana
zinatolewa kwa wanawake hivyo basi wanawake hawana budi kujikomboa kwa
njia ya ujasiriamali.mama amina alisema hayo wakati akitoa mada
alipowatembelea wanawake wa zanzibar walioniufaika na mradi wa manjano
dream makers ulio chini ya taasisi ya manjano foundation yaliomalizika
kwenye hotel ya mtoni marine zanzibar.

Mbunifu
wa mavazi Amina Design akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano
Foundation Mama Shekha Nasser Pamoja wa Baadhi ya wasaidizi Kutoka
Taasisi ya Manjano Foundation.
Akieleza
Zaidi Mama Amina Plummer Ambaye ni Mbunifu wa Mavazi amewaomba
wanawake wa Zanzibar Kupenda Ujasiriamali kwa Kuwa ni Kazi Pekee ambayo
kadiri Unavyoifanya kwa Juhudi na Maarifa Pia inasaidia Kuongezeka kwa
Kipato cahako.Hivyo wakina mama wa Zanzibar hawana Budi Kuchangamkia
nafasi hiyo ya kujifunza Ujasiriamali Kutoka Taasisi Ya Manjano
Foundation .

Washiriki wa Semina Hiyo kutoka Visiwani Zanzibar wakisikiliza kwa Makini Mda zilizokuwa zikitolewa kwenye Mafunzo hayo.