Ridhione
Senga (wa pili kushoto) ambae ni Mwenyekiti wa Madereva wa Daladala
wanaofanya shughuli zao katika barabara ya Bugarika-Mzunguko Jijini
Mwanza, jana akilalamikia suala la uwepo wa tax bubu linalowasumbua
katika shughuli zao.
Ramadhan Idd ambae ni Kaimu Mwenyekiti wa Madereva wa daladala za Bugarika-Muzunguko akitoa malalamiko yake.
Athuman Bin Malick ambae ni mmoja wa madereva wa daladala za Bugarika-Mzunguko Jijini Mwanza.
Kulia ni Kaptaini Michael Rogers ambae ni Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi wake
Alisema
licha ya madereva wa tax bubu wanaobeba abiria kama daladala katika
eneo wanalofanyia kazi hususani kubeba abiria wanaoenda na kutoka katika
hospitali ya Rufaa ya Bugando kuzuiliwa, bado madereva hao wa tax bubu
wameendelea na biashara hiyo kama kawaida.
Senga
alibainisha kwamba hatua hiyo inawaweka katika wakati mgumu katika
kutimiza majukumu yao kutokana na kupata hasara kila kukicha ambapo
amesema ikiwa itaendelea wataitisha mgomo ili kushinikiza kilio chao
kufanyiwa kazi.
"Sisi
tunalipa mapato, lakini jambo la ajabu hawa madereva wa tax bubu ambao
hawana leseni ya kubeba abiria wamekuwa ndio wanafanya kazi ya daladala
licha ya kupigwa marufuku katika kikao tulichokaa ijumaa iliyopita baina
ya Sumatra, halmashauri ya Jiji, Polisi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza pamoja na wawakilishi wengine bila kuwasahau viongozi wa daladala
na tax. Kama hali hii itaendelea tutafanya mgomo hapa na hakuna huduma
yoyote ya kubeba abiria itakayotolewa".Alisema Senga.
Ramadhan
Idd ambae ni Kaimu Mwenyekiti wa Madereva wa daladala za
Bugarika-Muzunguko Jijini Mwanza aliunga mkono hoja ya mwenyekiti huyo
na kusema kuwa ikiwa mamlaka husika zitashindwa kutatua suala la tax
bubu katika eneo hilo, wao watachukua hatua ya kusitisha huduma ya
usafirishaji katika barabara hiyo ya Bugarika-Buzuruga.
"Hizi
tax bubu tunasikia ni za wakubwa na ndiyo maana hawa madereva
wanaoziendesha wana jeuri mno. Sisi tunasema haya ni majipu na
tunawaomba viongozi wengine wakubwa akiwemo Mhe.Magufuli, waangalie huku
Jijini Mwanza maana kuna majipu makubwa ya kutumbua".Alisema Athuman
Bin Malick ambae ni mmoja wa madereva wa daladala za Bugarika-Mzunguko
Jijini Mwanza.
Kaptaini
Michael Rogers ambae ni Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoani Mwanza,
ameshauri suala hilo kutatuliwa na jeshi la polisi kitengo cha usalama
barabarani kwa kuwa ndilo lenye jukumu la kukamata vyombo vya usafiri
vinavyofanya kazi kwa kukiuka sheria na taratibu zilizoweka na mamlaka
husika ikiwemo halmashauri ya Jiji Mwanza ambayo ndiyo inasimamia
taratibu la utendaji kazi wa tax.
Juhudi
za kuwatafuta madereva wa tax hizo zinazodaiwa kufanya kazi kinyume cha
sheria (tax bubu) bado zinaendelea ili kujua kuzungumzia malalamiko
yanayowakabiri.
.Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo