Feb 6, 2016

Maafa: Tetemeko Kubwa la Ardhi Laikumba Taiwan

Tetemeko Taiwan (1)
Tetemeko kubwa la ardhi limeikumba nchi ya Taiwan, usiku wa kuamkia leo na kuangusha majengo kadhaa likiwemo jengo la ghorofa 17 ambapo hadi sasa watu watano wamethibitishwa kufariki dunia.
Tetemeko hilo la kipimo cha Ritcher 6.4 lilitokea karibu na mji wa Tainan.
Zaidi ya watu 200 wameokolewa kutoka kwa jengo hilo, ingawa waokoaji wangali wanajaribu kuwafikia watu wengine ambao inadhaniwa wangali wamekwama katika mabaki ya jengo hilo.
Tetemeko hilo liligonga usiku wa manane wakati watu wengi walikuwa wamelala.
Kumetokea matetemeko mengine madogo matano mda mfupi baada ya tetemeko hilo kuu.
Idara ya kusimamia maswala ya chini ya radhi inasema kuwa tetemeko hilo lilitokea sehemu ya juu pekee, hali ambayo husababisha madhara makubwa zaidi Tetemeko Taiwan (2) Tetemeko Taiwan (3) Tetemeko Taiwan (4) Tetemeko Taiwan (6) Tetemeko Taiwan (7) Tetemeko Taiwan (8) Tetemeko Taiwan (9) Tetemeko Taiwan (10) Tetemeko Taiwan (11) Tetemeko Taiwan (12) Tetemeko Taiwan (13) Tetemeko Taiwan (14) Tetemeko Taiwan (15) Tetemeko Taiwan (16) Tetemeko Taiwan (17)