Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy.
MAMLAKA ya Mawasiliano TCRA imevifungia vituo 21 vya Radio na 6 vya TV kwa kushindwa kulipa kodi ya lesseni kwa wakati.
Akitangaza uamuzi huo, Mkurugenzi wa
Habari na Mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy, amesema vituo hivyo
vimefungiwa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Jumatatu ya January 18
mwaka huu na kwamba mitambo ya vituo hivyo itazimwa ifikapo kesho saa 6
usiku (yaani Jumapili usiku kuamkia Jumatatu), na itawashwa baada ya
vituo hivyo kulipa madeni yanayowakabili.
Mungy amesema mamlaka hiyo haiwezi
kusema ni kiasi gani cha pesa ambacho vituo hivyo vinadaiwa kwa madai
kuwa kanuni na taratibu haziwaruhusu kutaja kiasi hicho kwa kuwa ni siri
kati ya TCRA mteja.
Aidha Mungy amesema kuwa TCRA imewataka
wadau wote wa mawasiliano nchini kutii sheria bila shuruti na kufuata
taratibu, huku akisisitiza kuwa zoezi hilo la kuwasaka wanaokwepa kodi
ni endelevu.
1. Sibuka FM2. Breez FM
3. Country FM
4. Ebony FM
5. Hot FM
6. Impact FM
7. Iringa Manicipal TV
8. Kiss FM
9. Kitulo FM
10. Kifimbo FM
11. Mbeya City municipal TV
12. Radio 5
13. Radio Free Afrika
14. Musa Television Network
15. Pride FM Radio
16. Radio Huruma
17. Radio Uhuru
18. Star TV
19. Rock FM Radio
20. Standard FM Radio
21. Sumbawanga Municipal TV
22. Tanga City TV
23. Top radio FM limited
24. Ulanga FM