Jan 16, 2016

MWILI WA MTOTO ALIYE SOMBWA NA MAFURIKO MWANZA WAPATIKANA.

Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza wakitoka eneo la  Kamanga Feri jijini hapa huku wakiwa wameubeba mwili wa mtoto Janet James, mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mabatini uliopatikana mara baada ya wavuvi kuuona ukielea kando kando ya ziwa Victoria eneo la Kamanga Feri. 
 Wavuvi hao wanaeleza kuwa waliuona mwili wa mtoto huyo ukielea, na kutokana na taarifa za kuzama kwake walizozipata kutoka kwenye vyombo vya habari mbalimbali jijini Mwanza ikiwemo Jembe Fm, pamoja na taarifa za wasimamizi wao kibiashara kwenye mwalo huo nao hawakusita kutoa taarifa haraka kwa jeshi la polisi kwaajili ya hatua zaidi.