Jan 26, 2016

ETIHAD YAZINDUA HUDUMA ZA SAFARI ZA NDEGE KUFIKA MJI MKUU WA MOROCCO, RABAT.

Ndege ya uzinduzi ya Shirika la Ndege la Etihad ikipokelewa na magari ya zimamoto ambayo yalimwaga maji kuashiria uzinduzi rasmi wa Safari za ndege kati ya Rabat na Abudhabi. 

Safari kati ya Abu Dhabi na Morocco kufikia tisa kwa wiki 
Shirika la ndege la Etihad lazindua rasmi huduma zake za ndege baina ya Abu Dhabi na Rabat, Morocco, ikiwa ni kituo chao cha pili nchini humo.

Ndege ya uzinduzi iliwasili mchana wa leo uwanja wa ndege Sale-Rabat na kupokelewa na mzinga wa maji kama ilivyo desturi ikifuatiwa na wageni rasmi kuwasili, wakiwemo; Lahcen Haddad (Waziri wa Utalii Morocco), na Balozi wa UAE kwa Morocco, Mh. Al Asri Saeed Al Dhaeri.

Huduma hii itakayopatikana mara mbili kwa wiki kupitia ndege aina ya Airbus A340-500 itakuwa yakipekee baina ya Rabat na Abu Dhabi. Tayari kukiwa na safari baina ya Abu Dhabi na Casablanca, shirika litafikisha jumla ya safari tisa kwa wiki kwenda nchini Morocco

Ndege ya uzinduzi (EY615) kwenda Rabat ilibeba msafara ulioongozwa na Khaled Al Mehairbi, Makamu Rais Mambo ya Serikali na Siasa za Anga. Uwakilishi huu ulijumuisha Kapteni Salah Awadh Alfarajalla, Makamu Rais Usalama na Maaendeleo ya Waendesha Ndege Kitaifa; Hareb Mubarak Al Muhairy, Makamu Rais Mambo ya Mashirika na Kimataifa; Ali Al Shamsi, Makamu Rias Operesheni za Kitovu cha Abu Dhabi; Joost Den Hartog, Kaimu Makamu Rais wa Mauzo Duniani; na Amer Khan, Makamu Rais Mashariki ya Kati na Africa Kaskazini.

James Hogan, Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Etihad, alisema shirika limefurahishwa na uzinduzi wa huduma ya Rabat kama kituo cha pili katika safari za Morocco.

“Safari hizi mpya zitakazounganisha miji hii zinadhihirisha dhamira ya Etihad kuendelea kujenga mahusiano endelevu na kanda ya ksakazini mwa Afrika na kuimarisha uhusiano kati ya Morocco na Umoja wa Falme za Kiarabu,” alisema.

“Rabat ni mji wa kihistoria unaovutia wanaosafiri kwa ajili ya burudani na biashara. Kwa kupitia huduma yetu mpya, tunalenga kutumia mtandao wetu uliopo duniani kote kukuza wingi wa wasafiri wataotumia njia hii kuingia Morocco. Vivyo hivyo tunarahisisha safari katika Rabat hadi Abu Dhabi pamoja na miji mingine tunayofika, huku tukiwapa wageni wetu fursa ya kufurahia huduma zetu za viwango vya juu zinazotambulika dunia nzima.”

Pamoja na Casablanca, huduma hii ya Rabat itafikisha jumla wasafiri 4,200 kila wiki kwenda Morocco.

Kama UAE, serikali ya Morocco imewekeza sana katika kuiendeleza sekta ya utalii. Mwaka 2010, serikali ilizindua Vision 2020 ikiwa na mpango wa kuifanya Morocco kuwa kati ya sehemu kuu 20 za utalii duniani na hii itachangia kuongeza idadi ya watalii hadi mara mbili ya idadi ya awali hadi kufikia takribani milioni 20 mpaka kufika mwaka 2020.