
Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma,SSP Nuru Selemani
akiwakiwaelimisha abiria ndani ya basi lilofanya safari zake mikoani
ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu
kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya
moto.Kampeni hiyo inadhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Askari
wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma SGT.
Tunu Kuta(kulia) akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la
kwenda mikoani, Masoud Seleman ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to
Send”inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la
polisi kitengo hicho katikati Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa
huo SSP Nuru Selemani na wapili kulia ni Kaimu mkuu wa kanda ya kati wa
Vodacom Tanzania,Heladius Kisiwani.

Kaimu
mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania,Heladius
Kisiwani(kulia)akimpa maelezo dereva wa basi liendalo mikoani,Masoud
Selemani kuhusiana na pete ya kidoleni inayotolewa na Kampuni hiyo kwa
kushirikiana na jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani yenye
ujumbe“Wait To Send” unaohamasisha madereva wa vyombo vya moto
kutokutumia simu za mkononi wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Zoezi hili
lilifanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mkoani cha
Dodoma.Katikati Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma,SSP
Nuru Selemani.

Mkuu
wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao
makuu ya Polisi ASP,Abel Swai akitoa elimu kwa abiria ndani ya basi
liliendalo mikoani katika stendi kuu ya mabasi Dodoma ikiwa ni sehemu ya
mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva
kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni
hiyo inadhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma,SSP Nuru
Selemani(kulia) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari(hawapo
pichani)Kuhusiana na mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa
elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia
vyombo vya moto.Kampeni hiyo inadhaminiwa na Vodacom Tanzania.Wengine
kutoka kusho ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu na
Kaimu Mkuu wa kanda ya kati wa kampuni hiyo Heladius Kisiwani.

Baadhi
ya Madereva wa mabasi yanayosafirisha abiria mikoani wakimsikiliza
Kaimu Mkuu wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania,Heladius Kisiwani(kulia)
akiwapatia elimu kuhusiana na mwendelezo wa kampeni ya”Wait to
Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote
wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inaendeshwa na Jeshi la polisi la
Usalama barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.

Shughuli
ikiendelea ya kutoa elimu kuhusiana na mwendelezo wa kampeni ya”Wait to
Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote
wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inaendeshwa na Jeshi la polisi
la Usalama barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.
Kampeni ya usalama barabarani ya kuwataka
madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani,leo imefanyika
katika Mkoa wa Dodoma.
Madereva wameendelea kuhimizwa kutotumia
vinywaji vyenye ulevi na kuacha tabia ya kuongea na simu au kutuma na
kupokea ujumbe wa maneno (sms) wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Mkoa
wa Dodoma, SSP Nuru Selemani amesema kampeni hii ni muhimu katika
kupunguza matukio ya ajali “Watumiaji wa barabara hii ya mkoa wa Dodoma
ni wengi hususani madereva wa vyombo vya moto hawana budi kuzingatia
maelekezo ambayo tumekuwa tukiwapa katika kampeni hizi ili tupate
matokeo mazuri kwa kupunguza ajali kama ilivyokusudiwa”Alisema
Alisema madereva wakizingatia sheria za
barabarani kwa kiasi kikubwa ajali zinazoendelea kutokea kila siku
zitapungua hususani katika kipindi hiki cha msimu unakoelekea wa sikukuu
na aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuunga mkono jitihada za serikali
katika kupambana na tatizo hili ambalo limekuwa sugu .
Kwa upande wake,Kaimu Mkuu wa kanda ya kati
wa asoko wa Vodacom Tanzania Heladius Kisiwani, alisema Vodacom
itaendelea kushirikiana na serikali katika kuunga mkono jitihada za
kuondoa matatizo kwenye jamii kama lilivyo tatizo hili la ajali ili
kuhakikisha wananchi wanaishi maisha murua na marefu.”Tunatoa rai kwa
madereva wote kuzingatia sheria za barabarani na kutokutumia simu wakati
wowote wakiwa wanatumia vyombo vya moto”.
Aliongeza kuwa Vodacom itakuwa mstari wa
mbele kuelimisha jamii athari za kuendesha gari wakati huo huo unatumia
simu ya mkononi kupitia kampeni ya “Wait to Send” pia itaendelea
kuhamasisha madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Alisema kampuni hiyo itaendeleza kutoa
elimu kwa mikoa mingine pia katika uhamasishaji wa madereva kuzingatia
sheria za barabarani katika miji ya Morogoro,Dar es Salaam na mikoa
mingine na kampeni hizi zitaendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini.
Katika kampeni ya leo wafanyakazi wa
Vodacom kwa kushirikiana na askari wa usalama barabarani walitoa
uhamasishaji kwa madereva kuacha kuongea na simu wanapoendesha vyombo
vya moto na kuwagawia madereva pete maalum za kuwatahadharisha kutotuma
ujumbe wa simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto pia
zoezi la kupima madereva kubaini kama wanatumia vilevi lilifanyika
ambapo wadereva waliokutwa wanaendesha vyombo vya moto walichukuliwa
hatua kali za kisheria.
Baadhi ya abiria walioshuhudia kampeni hii
mkoani Dodoma wamesema ni ya muhimu itasaidia kupunguza ajali
nchini.”Hivi sasa ajali nyingi zinazotokea hapa nchini zinasababishwa na
uzembe wa madereva,kampeni hizi zikiendelea zitapunguza ajali kwa kiasi
kikubwa”.Alisema Sunday Israel mkazi wa Dodoma aliyekuwa safarini
kuelekea Singida