Rais Dk. John Pombe Magufuli leo
ameendelea na oparesheni yake ya ‘Kutumbua Majipu’ baada ya kuvunja Bodi
ya Bandari (TPA) na kutengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Bandari nchini Bw. Awadhi Masawe.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Bw. Awadhi Massawe.
Pia rais amemfukuza kazi Katibu Mkuu
Wizara ya Uchukuzi Dkt Shabani Mwinjaka na maofisa wengine nane wa
Mamlaka ya Bandari na kuwagiza polisi wawakamate wote na kuwaweka chini
ya ulinzi.
Massawe aliteulia na Waziri wa Uchukuzi
Msitaafu, Samwel Sitta kushikila nafasi ya Mhandisi Madeni Kipande
aliyesimamishwa kwa tuhuma za utendaji mbovu ili kupisha uchunguzi