
Dkt.
Magufuli (katikati) akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Nyamagana (pichani
kulia) Ndugu Stanslaus Mabula mbele ya Maelfu ya wakazi wa jiji la
Mwanza kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Furahisha jioni ya
leo.Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza waliohojiwa na Globu ya Jamii
walieleza na kukiri wazi kuwa haijawahi kutokea kwa mapokezi haya
makubwa na ya aina yake,na kuwa Magufuli ndiye anaetosha kuvaa viatu vya
Urais.

Dk Magufuli (katikati) akiwanadi Mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela, Anjela Mabula

Dk Magufuli (katikati) akiwanadi Mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela, Anjela Mabula na Stanslaus Mabula ambaye anagombea ubunge Jimbo la Nyamagana.

Maelfu
ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika
mithili ya Utitiri kwenye uwanja wa Furahisha jioni ya leo kwenye
mkutano wa kampeni,ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli
aliwahutubia na kuwaomba wampigie kura za kutosha ifikakapo Oktoba 25
kwenye uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.

Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia Maelfu ya wakazi wa
jiji la Mwanza na vitongoji vyake katika viwanja vya Furahisha jioni ya
leo jijini Mwanza kwenye mkutano wa kampeni,ambapo Mgombea Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi
CCM,Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia na kuwaomba wampigie kura za
kutosha ifika Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.


Sehemu
ya umati wa wakazi wa jiji la Mwanza wakishangilia jambo wakati Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akizinadi sera zake.

sehemu ya umati wa watu ndani ya viwanja vya furaisha jijini Mwanza jioni ya leo.
Wananchi
wakiuzuia msafara wa Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kupitia CCM, Dk John Pombe Magufuli uliokuwa ukisindikizwa na umati wa
watu kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwenda kwenye mkutano wa kampeni
katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
Wananchi
wa Jiji la Mwanza wakiwa wametandika vitenge kwenye lami ili msafara wa
Dk Magufuli upite kuelekea kwenye mkutano wa Kampeni katika viwanja vya
Furahisha jioni ya leo jijini Mwanza.
Mgombea
urai wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwapungia mkono
wananchi alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja
vya Furahisha, jijini Mwanza

Mgombea
urai wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwapungia mkono
wananchi alipokuwa akiwaaga baada ya mkutano wa kampeni kumalizika
katika viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza


Msafara
wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John pombe Magufuli ukiondoka katika
viwanja vya Furahisha jioni ya leo mara baada kumaliza mkutano wa
kampeni,huku ukisindikizwa na umati mkubwa wa watu.
