Kampuni
ya mawasiliano ya Vodacom imepata tuzo ya kuwa mwajiri bora katika
sekta ya mawasiliano pia ipo miongoni mwa makampuni kumi bora yanayotoa
ajira na kuwa na mazingira bora kwa wafanyakazi wake nchini Afrika ya
Kusini kwa mwaka 2015.
Hafla
ya kutangaza makampuni yanayoongoza kwa ajira nchini Afrika ya Kusini
ilifanyika jana katika eneo la Gallagher Estate mjini Jahannesburg
ambapo Vodacom ilitangazwa kuwa miongoni mwa makampuni 10 bora
yanayoongoza katika ajira na kwa kufuata taratibu na kanuni za raslimali
watu na ilitangazwa kuwa kampuni inayoongoza kwa kufuata misingi bora
ya ajira katika sekta ya mawasiliano.
Tuzo
ya waajiri bora ni mpango ambao huandaliwa kila mwaka na makampuni
yanayoongoza kwa kufuata sheria na misingi bora ya ajira na raslimali
watu hutangazwa na kupewa tuzo.
Akiongea baada ya
kupata tuzo hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Raslimali watu wa Vodacom
Matimba Mbungela alisema:”Tumewekeza kwa kisi kikubwa katika uendeshaji
wa shughuli za raslimali watu katika kampuni yetu kuanzia teknolojia na
kuweka mifumo bora inayokubalika kimataifa ambayo
inatoa mwanya kwa wafanyakazi wetu kufanya kazi katika mazingira mazuri
na kampuni kuendesha shughuli zake kwa ufanisi mkubwa”.
Mbungela alisema kuwa tuzo hii inatoa taswira halisi ya kampuni yetu kwa kuwa kuwa mwajiri bora kunaendana sambamba na kutoa huduma bora kwa wateja.
Tuzo hii imetolewa kwa Vodacom baada ya kubainika kuwa inafuata na
kutekeleza kanuni na taratibu za raslimali watu zinazokubalika
kimataifa na imekuwa mstari wa mbele kuajiri wafanyakazi wazuri na
kuendeleza vipaji vyao.