Ndugu na marafiki wakipeleka mauwa kwenye kaburi la Carrey (halipo pichani). 
Marehemu Cathriona White akiwa na aliyekuwa mpenzi wake, Jim Carrey.
Ireland, Uingereza
CATHRIONA WHITE (28) mkazi wa visiwa vya
Ireland, Uingereza, aliyesadikiwa kujiua Jumatatu iliyopiyta baada
'kutemwa' na mpenzi wake ambaye ni mwigizaji maarufu wa filamu za
Hollywood, Jim Carrey amezikwa nyumbani kwao visiwa vya Ireland katika
makaburi ya familia. Cathriona amezikwa jilani na kaburi la maerehemu
baba yake Pat.
Msiba huo umehudhuriwa na ndugu, jamaa
na marafiki wengi akiwemo Jim Carrey aliyesafiri kutoka marekana
hadi visiwa vya Ireland kwa ndege binafsi jana.
Siku moja kabla ya kifo chake, Cathriona
aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kuwa, “Ninajiondoa kwenye
mtandao wa Twitter, nimekuwa mwema kwa marafiki zangu na mpenzi wangu.”
Cathriona na Carrey walianza uhusiano
mwaka 2012, lakini baadaye walifarakana na kuachana baada ya miezi
michache. Mwaka 2014 walirudiana wakaendelea na mahusiano kwa muda wa
wiki mbili tu kabla ya kuachana tena. Mei mwaka huu marafiki hao
walirudiana tena kwa mara nyingine ndipo walipokuja kuachana tena hivi
karibuni.
chanzo: Daily mail