MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI KWENYE TAMASHA LA MAJIMAJI SELEBUKA 2015
Kikundi
cha Jakaya Sanaa kilichoibuka bingwa wa shindano la Ngoma za Asili
kwenye Tamasha la Majimaji Selebuka 2015 yanayoendelea kwenye Uwanja wa
Makumbusho ya Mashujaa ya Vita vya Majimaji, Songea.
Kikundi
cha Ngoma cha Lihanje-Ngoma ya Mganda wakifanya yao katika Shindano la
Ngoma za Asili kwenye tamasha la Majimaji Selebuka 2015.Jaji
Mkuu katika Shindano la Ngoma za Asili, Balthazar Namusya akimvisha
Medali ya Shaba mkuu wa Kikundi cha Ngoma cha Lihanje Ngoma ya Kioda
kilichoshika nafasi ya tatu kwenye Tamasha la Majimaji Selebuka.
Mmoja
wa Wanakikundi cha Jakaya Sanaa, akipokea zawadi ya fedha taslim,
medali ya dhahabu na cheti kama bingwa wa shindano la Ngoma za Asili
katika Tamasha la Majimaji Selebuka 2015 linaoendelea kwenye Uwanja wa
Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji, Songea.
Majaji
wa Ngoma za Asili wakiwa na vyeti vyao walivyotunukiwa katika Tamasha
la Majimaji Selebuka 2015, linaloendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho wa
Mashujaa wa Vita vya Majimaji mjini Songea. Tamasha hilo limeratibiwa na
Asasi ya Somi.
Mkurungenzi
mwenza wa Asasi ya Somi, Dk Damas Ndumbaro wa pili kutoka kushoto
akifuatilia kwa ukaribu Shindano la ngoma za asili katika tamasha la
kila mwaka la Majimaji Selebuka 2015 kwenye Uwanja wa Makumbusho wa
Mashujaa wa Vita vya Majimaji, Songea.
Wasanii
kutoka vikundi vitatu tofauti vilivyofanikiwa kuingia fainali ya
shindano la Ngoma za Asili katika tamasha la majimaji selebuka wakiwa
katika picha ya pamoja baada ya
kutunukiwa zawadi zao. Tamasha hilo
linaendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho wa Mashujaa wa Vita vya
Majimaji, Songea.