
Magufuli akiongea na umati uliofurika katika kijiji cha Nduguti, Jimbo la Iramba mashariki.

Magufuli akiongea na wakazi wa Misigiri.

Magufuli
akiwahesabia push- up wagombea wake wa ubunge kutoka kushoto Lazaro
Nyalandu, Musa Sima, Mwigulu Nchemba na Mbunge mstaafu Capten John
Chiligati.

Mbunge
wa zamani wa Singida Mjini Mohamed Dewj akiwaaga wananchi
waliokusanyika viwanja vya Peoples Singida mjini na kuwaahidi kuendelea
kuwasaidia.

Mbunge
za zamani wa Singida mjini, Mohamed Dewj akimpa hai magufuli baada ya
kutangaza kumuunga mkono mbunge mpya anayegombea jimbo hilo.

Mohamed Dewj na Lazaro Nyarandu wakipeana hai.

Mwigulu
Nchemba akinyoosha mikono kwa furaha baada ya Magufuli kuwatangazia
wanachi wa kiomboi, jimbo la Iramba Maghalibi wamchague mbunge huyo.

Temba (kushoto) na Chegge wakikamua katika viwanja vya Peoples.

Mwana Bongo fleva, Frejoo akikamua kabla ya Magufuli kuanza kumwaga sera.

Wakazi wa Kijiji cha Sepuka wakiwa juu ya gari ili wamuone vizuri Magufuli baada ya kusimamishwa na wakazi wa kijijini hicho.

Wanausalama wakiwa kwenye moja ya paa iliyopo karibu na uwanja wa Peoples ili kuimarisha usalama wakati Magufuli akimwaga sera.

Sehemu ya umati uliojitokeza uwanja wa Peoples Singida mjini kumsikiliza Magufuli.

Sehemu ya wakazi wa Kiomboi wakisikiliza sera za Magufuli.
Mgombea urais kupitia CCM John Magufuli leo Jumamosi ameendelea na
kampeni za kuomba kura mkoani Singida ambapo baadhi ya maeneo aliyofanya
mikutano ya kuomba kura ni pamoja na Kijiji cha Sepuka, Kikonge, Ndago,
Misigiri, Kiomboi, Sibiti, Wilaya mpya ya Mkalama, Nduguti, Nkungi,
Singa, Mtinko, Ilongero na kumalizia katika Uwanja wa Peoples uliopo
Singida mjini ambapo mkutano huo ulisababisha barabara kadhaa zilizo
karibu na uwanja huo kutopitika na vyombo vya usafiri kufuatia kufurika
umati mkubwa uliokuwa ukizidi kumiminika kadili Magufuli alivyokuwa
akiendelea kumwaga sera.
Akizungumza na wakazi mbalimbali kwenye maeneo aliyofanya mikutano ya
leo Magufuli aliwaahidi vijana kupata ajira katika serikali yake
kupitia sera yake ya uanzishaji viwanda pamoja na kutoa ajira serikalini
bila upendeleo wala visingizio vya uzoefu kazini.
Magufuli aliwalaumu viongozi wenye tabia ya kuwawekea kauzibe vijana
wanaotoka masomoni na kuwaambia hawawezi kuajiriwa mpaka wawe na uzoefu
kazini jambo ambalo linawakwamisha wasomi wengi wanaotoka masomoni.
Amesema katika utawala wake ukitoka masomoni unafikia ajira ilimradi uweze kuimudu.
Pamoja na ajira kwa vijana Magufuli aliwaahidi wakazi wa vijiji
alivyotembelea kuwa atazidi kusambaza umeme katika vijiji ambavyo
haujafika na kutatua tatizo la maji mkoani humo ambalo lilishaanza
kutatuliwa na uongozi uliopita lakini yeye ataboresha zaidi suala hilo.
Kila alipotembelea mgombea huyo alishangiliwa na umati wa watu wa
vyama mbalimbali hasa alipotangaza ilani ya chama chake ya kutoa elimu
bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne na pale alipotangaza
serikali yake ikiingia madarakani kutoa mikopo kwa vikundi vya kina mama
na vijana kwa kila kijiji na kila kata nchi nzima.
Magombea huyo pia alisema serikali ya chama chake juzi Alhamisi
kimepokea msaada wa shilingi bilioni 992 kutoka Marekani kwa ajili ya
miradi ya maendeleo hivyo wananchi wakae mkao wa neema endapo
atachaguliwa kuingia ikulu.
Mwisho Magufuli aliwaasa wakazi wa
Singida kutoichezea bahati hiyo kwa kuwachangua viongozi wa vyama vya
upinzani na kuataka wamchague kwenye urais na kuwapa ubunge wagombea wa
CCM na Madiwani.
(Habari Picha:Richard Bukos) GPL,WAMBURA BABU BLOG/MICHUZI MEDIA