Oct 19, 2015

Diamond kuachia nyimbo 3 kabla mwaka haujaisha


12107505_1660640227516381_1029669344_n
Diamond Platnumz amedai kuwa kabla mwaka huu haujaisha atakuwa ameachia nyimbo 3 mpya. Diamond alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni wakati ya mapokezi yake katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea Marekani alikoshinda tuzo za Afrimma.
“Nimeuambia uongozi kabla ya mwezi wa kwanza hapa katikati ziwe zimeshatoka hata ngoma tatu za moto kabisa,” alisema Diamond.
Tayari muimbaji huyo amesharekodi nyimbo kadhaa za kolabo ukiwemo wimbo aliowashirikisha P-Square na Ne-Yo.

credit: Bongo5