Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Wakati shule zote za serikali na za binafsi nchini Kenya zikianza
kufungwa kuanzia hii leo, rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta akihutubia
taifa hilo kwa njia ya televisheni amesisitiza kuwa serikali yake haina
uwezo wa kulipa nyongeza ya mishahara wanayodai waalimu wanaoendelea na
mgomo.Barua kutoka kwa wizara ya elimu imeagiza shule zote za serikali na za kibinafsi zifungwe na wanafunzi warudi majumbani mwao. Watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.