Kala Jeremiah anaamini kuwa hatua ya Baraza la Sanaa Taifa, BASATA kuifungia ngoma ya Roma Mkatoliki ‘Viva Roma’ ni sawa na kuingilia na kuvuruga demokrasia Akizungumza na kipindi cha The Jump Off cha Times FM, Kala alisema kama tatizo ni ushahidi wa kile alichokiimba Roma,nyimbo zote zinapaswa kufungiwa kwa kuwa hazina uhalisia.
“Ushahidi gani unautaka?” alihoji. “Tuseme basi wale wanaoimba ‘baby nakuona kwenye glass’ watoe ushahidi wao wanamuonaje mtu ndani ya glass? Sababu uimbaji ni unakuwa na fikra kwanza. Nafikiri BASATA wameingilia na wanavuruga demokrasia kwenye mziki wetu kuwanyima watu uhuru wa kuongea. Walianza kwa vitisho zamani, kuzifungia kimya kimya sasa hivi ndio wameleta hii ya kuzifungia waziwazi kabisa.”
credit: Bongo5