Navy Kenzo wanaendelea kula matunda ya juhudi zao katika muziki, ambapo uwekezaji walioufanya kwenye video yao ya ‘Game’ unaendelea kuzaa matundaHatimaye hit song yao ‘Game’ imefanikiwa kupanda hadi namba 1 wiki hii kwenye chati ya video bora za Afrika, ‘Official African Chart’ ya kituo cha MTV Base.
Hadi sasa ‘Game’ imewafungulia Navy Kenzo njia nyingi za mafanikio ya kufahamika barani Afrika, na kuingia kwenye chati mbalimbali za vituo vikubwa. Mbali na MTV Base, video hiyo iliyoongozwa na director wa Afrika Kusini, Justin Campos imeshaingia kwenye chati nyingine mbalimbali za vituo vya Nigeria ikiwemo Soundcity na kufika hadi nafasi ya 1.