Sep 27, 2015

DMX aachiwa kutoka jela, lakini anaweza kurudishwa tena!


dmx-2012
Rapper DMX ameachiwa huru kutoka jela siku ya Ijumaa Sept 26 japo kuna uwezekano wa kurudishwa ndani muda wowote tena. Mwezi July rapper huyo alihukumiwa miezi sita jela baada ya kushindwa kulipa matumizi ya mtoto, lakini alijitetea kuwa hakufahamu kama mwanamke aliyezaa naye alikuwa akimdai pesa yoyote, kwa mujibu wa TMZ.
Licha ya kuwa ameachiwa, lakini endapo jaji atathibitisha kuwa alikuwa anafahamu kuwa ana jukumu la kulipa matumizi ya mtoto na bado hakutimiza wajibu huo makusudi, atalazimika kurudishwa jela kumalizia kifungo chake.