
Kaimu
Mkurungenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Michael
Mhando na Mkuu wa Huduma za Matibabu Jeshini,Brigedia Denis Raphael
wakitia saini Mkatamba wa Ushilikiano leo katika Makao Mkuu ya Jeshi
Jiji Dar es Salaam.

Kaimu
Mkurungenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Michael
Mhando na Mkuu wa Huduma za Matibabu Jeshini,Brigedia Denis Raphael
wakibadilishana hati za makubaliani leo katika Makao Mkuu ya Jeshi Jiji
Dar es Salaam.
WANACHAMA kutibiwa katika hospitali za jeshi,
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeingia mkataba na Jeshi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) ambapo wanachama wa mfuko huo na wategemezi wao
watapata huduma za matibabu katika hospitali za jeshi nchini kote.
Mkataba
huo wa miaka mitatu uliosainiwa jana unalenga kupanua wigo wa vituo vya
matibabu na kuanzisha ushirikiano wa kihistoria baina ya pande mbili
hizo.
Akizungumza
wakati wa kutia saini mkataba huo Mkuu wa Huduma za Afya Jeshini
Brigedia Denis Raphael Janga, amesema amepokea kwa furaha mkataba huo
kwa kuwa utawapa nafasi ya kutoa huduma bora kwa kundi kubwa la
wanachama wa NHIF ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikosa huduma katika
vituo vya jeshi vilivyo karibu nao.
Ameahidi
kushirikiana kwa karibu na uongozi wa NHIF ili kuhakikisha wanachama na
wategemezi wao wanapata vipimo na dawa wakati wote watakapokwenda
kwenye vituo hivyo.
Naye
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Michael
Mhando amesema NHIF kwa muda mrefu fursa ya kufanya kazi na JWTZ katika
sekta ya matibabu na kwamba mkataba huo unafungua historia mpya ya
ushirikiano baina ya taaisi hizo wa kujenga nchi kwa pamoja.
Amesema
ili kuhakikisha kuwa mkataba huo unakuwa na manufaa kwa pande zote
mbili Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya utaandaa mafunzo maalumu kwa watoa
huduma wa vituo vya jeshi ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na uelewa wa
pamoja wa namna ya kuhudumia wanachana wa NHIF watakaokwenda kupata
huduma katika vituo hivyo.
Mhando
ameongeza kuwa NHIF itaendelea kushirikiana na uongozi wa JWTZ ili
kukamilisha taratibu za kiutawala zitakazowawezesha wanaejeshi na
familia zao kujiunga na kunufaika na matibabu kupitia Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya.
Aidha
ameushauri uongozi wa JWTZ kutumia fursa ya mikopo ya vifaa tiba,
ukarabati na dawa na vitendanishi inayotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya ili kuhakikisha kuwa vituo vya matibabu vinavyomilikiwa na JWZT
vinakuwa na mazingira mazuri na vitendea kazi vinavyotakiwa.
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lina vituo vya matibabu vya ngazi mbalimbali zaidi ya kumi na nane nchini kote.