Wahamiaji wakiwa kwenye boti ndogo kabla ya kuokolewa.
Walinzi wa pwani ya Italia wameongoza shughuli ya kuwaokoa wahamiaji
2,000 ambao walituma ishara ya kuwa taabani kwenye mashua nje ya pwani
ya Libya.
Baadhi ya wahamiaji waliookolewa.
Bahari baina ya Libya na Italia, ndio njia inayotumiwa kwa muda mrefu
na wakimbizi kutoka Afrika na Mashariki ya Kati, ili kuingia
Ulaya.Umoja wa Mataifa umesema kuwa bahari ya Mediterranian ndio kivukio
maarufu.Kufikia sasa takribani watu laki moja wamewasili katika ufukwe
wa Italia, wengine zaidi ya laki moja na nusu waliwasili Ugiriki.
Meli ya Norway ikishiriki oparesheni hiyo.
Jarida moja la Norway, Aftenposten limesema kuwa manuari ya kijeshi
ya taifa hilo, Siem Pilot liko njiani kuwasaidia wahamiaji hao walioko
mashakani, Manuari hiyo iliwaokoa wahamiaji 320 mapema leo kabla ya
kurejeshwa tena kushiriki operesheni hiyo ya kuokoa nafsi za watu
wanaokisiwa kuwa takriban 3,000.
(Chanzo: BBC)