Nicas Ngumba Program Manager wa Restless Revelopment
Amabilis Batamula kutoka FEMINA Hip
“Fema imekuwa mstari wa mbele katika harakati za ukombozi wa vijana, tumekuwa tukielimisha vijana mbalimbali kupita majarida yetu. Femina Hip pamoja na asasi za kiraia tunazoshirikiana nazo tunaamini kwamba mara nyingi wasichana wanatengwa katika ulingo wa siasa kutokana na tamaduni na desturi zetu, taratibu za kidini, dhana na mitazamo ya jamii, ubaguzi wa kijinsia, kiwango kidogo
cha elimu, kutokuwa na taarifa, na athari za umasikini zinazowakumba wanawake, ili kujenga Tanzania njema, imara na itayokuwa,” alisema Amabilis Batamula.
Kwa upande wake naibu katibu mtendaji wa taasisi ya TYVA, Saddam Khalfan alisema katika uchukuaji wa maoni waligundua kuwa zaidi ya 80% ya vijana wamejiandikisha na wapo tayari kupiga kura.
“Unajua uchaguzi uliopita vijana wengi hawakupiga kura lakini mwaka huu wengi wameonyesha nia ya kutaka kupiga kura ili kuwapata viongozi wataowaletea maendeleo,” alisema.
Katika hatua nyingine baada ya uzinduzi huo wadau kama Mike Mushi ambaye ni mwanzilishi mwenza wa Jamii Forums, Maria Sarungi Tsehaim mwanzilishi wa Change Tanzania, Adam Anthony wa program OSIEA, rapper Nick wa Pili, Lawrence Chuma, mwanzilishi wa Tanzania Bora Initiative pamoja na Dr Ally Possi ambaye ni mwanasheria walipata wasaa wa kuizungumzia ajenda ya (What do we want see in Tanzania in the coming five year?).
Maria Sarungi wanzilishi wa Change Tanzania
Dr Ally Possi akizungumza na vijana
Lawrence Chuma kutoka Tanzania Bora Initiative
Margaret Mliwa wa Restless Development
Mike Mushi akizungumza na vijana
Vijana wa wakisikiliza kwa makini
Vijana wakitoa waoni yao juu wa serikali ijayo
Vijana wakiwa wamejitokeza kwa wingi
Wanafunzi kutoka Kambangwa sekondari