Aug 31, 2015

Maria Sarungi alia na ubabaishaji kwenye tasnia ya filamu


Maria Sarungi wanzilishi wa Change Tanzania
Mtayarishaji wa filamu na mwanaharakati maarufu nchini, Maria Sarungi amesema baadhi ya watu ndani ya tasnia ya filamu wamekuwa wakiwatumia wenzao kujinufaisha. Akizungumza wiki iliyopita kwenye uzinduzi wa ilani mpya ya vijana, Maria alisema tatizo la filamu kutowalipa wasanii ni tatizo la kiuchumi.

“Mimi nimefanya kazi na bodi ya filamu na pia ni mdau wa filamu na sanaa,” alisema. “Tatizo la filamu ni mapato basi, tutapeleka script pale film board atakwambia ulipe shilingi milioni moja sijui milioni mbili hatujui hiyo tukilipa itatulipa nini? Tatizo lililoko sasa hivi ambalo tunakabiliana nao ni uchumi,” aliongeza.
“Tutazungumza kila kitu lakini tatizo ni uchumi na katika filamu tatizo lake tunafanya kazi ambayo haishikiki, sanaa yetu haishikiki. Tatizo ni kuilinda kazi yako, na bahati mbaya kuna watu katika sekta hii wanatutumia. Ndio maana ndani yetu tunao uwezo wa kuzipekeka filamu zetu kimataifa ila tumekaa pembeni. Hakuna mazingira yaliyojengwa ya kuhakikisha kila mmoja ananufaika. Hata tukiendelea hatutafaidika mpaka mazingira haya yawekwe sawa,” alisisitiza Maria.

chanzo: Bongo5