Diamond akiwa studio jijini Johannesburg kuandika na kurekodi sehemu ya wimbo huo
Fresh kutoka kurekodi wimbo na Ne-Yo, Diamond Platnumz amekwea pipa kutoka Nairobi kwenda nchini Afrika Kusini kuungana na Mafikizolo kurekodi wimbo uitwao ‘Tell Every One’ ambao ni sehemu ya kampeni ya dunia ya kutokomeza umaskini, maradhi, njaa na matatizo mengine, The Global Goals. Mafikizolo tayari wameshaingiza sauti zao na aliyekuwa anakisubiriwa ni Diamond ambaye huenda leo akamaliza sehemu yake.
Studio Joburg South Africa Muda huu nikirecord nyimbo kwajili ya kutokomeza Umasikini Africa…. #TellEveryone #SustainableDevelopment @TheGlobalGoals,” ameandika Diamond kwenye picha aliyoweka Instagram.
S Africa's @MafikizoloSA studio in JHB today to #TellEveryone about @TheGlobalGoals. @diamondplatnumz in tomorrow! pic.twitter.com/KNG3sih8Vf
— The Global Goals (@TheGlobalGoals) August 20, 2015
Mchezaji wa Real Madrid, Gareth Bale naye ni sehemu ya mastaa duniani waliopo kwenye kampeni hiyo.
Gareth Bale tries the @TheGlobalGoals #DizzyGoals challenge 😂 (via: @GarethBale11) http://t.co/1GUBsA0g5f https://t.co/aB7ugTvGrw
— Bleacher Report UK (@br_uk) August 20, 2015
“On September 25th 2015, 193 world leaders will commit to 17 Global
Goals to achieve 3 extraordinary things in the next 15 years. End
extreme poverty. Fight inequality & injustice. Fix climate change.
The Global Goals for sustainable development could get these things
done. In all countries. For all people,” yanasomeka maelezo kwenye
tovuti ya Global Goals.